Jumanne, 31 Machi 2015

PICHA MBALIMBALI Z

WAGANGA WANAO ANDAMWA NA WANANCHI



Obert  funga.

Kahama.

31/03/2015.                      Waganga  wa kienyeji

Wakazi wa kijiji cha mwakata na Igugunwa  katika kata ya Isaka wilayani hapa mkoani shinyanga wamewalalamikia jeshi la polisi kwa azma ya kuwakamata waganga wa kienyeji wapiga ramli chonganishi huku wakiachwa waganga wa kienyeji 2 bila sababu yeyote.

licha ya serikali na wahisani mbalimbali kutoa misaada ya pesa,vifaa,vyombo na ujenzi wa nyumba za haraka kwa waadhirika wa majanga ya mvua ya mawe ilioikumba kijiji cha mwakata na Igugunwa kuua wananchi 48 na majeruhi 118 huku ikiwaacha wakazi 512 wakiwa hawana pa kuishi mpaka sasa utaratibu unafanyika wa kuwajengea eneo lenye maakazi.

Makizungumza kwa nyakati tofauti katika kijiji hicho walisema tupo katika kuweka jambo hili kwenye tahadhari ya waganga wa kienyeji waliosalia kwa mtafaluko uliokuwepo mwanzo kwa madai ya michango ya dua ya mvua iliochangishwa na waganga 2 kati ya kamati ya wazee 19 alisema Sofia Shija mkazi wa mwakata.

Awali kulikuwa na michango ya kamati ya wazee waomba dua ya mvua tokea 23/01/2015 ambayo kamati ina wazee 19 iliotufanya tuchange michango mbalimbali zaidi ya mara 3 kwa wachangishaji waliotuletea tangazo la kikao cha dua ya mvua.alisema Bi,Sofia

Naye Shabani ng’anghu mkazi wa kijiji hicho alisema hasira ya mganga wa kienyeji [mwanamaria]aliyeuawa na wanakijiji kwa kutoongea ukweli wa jambo la kuchangisha michango ya mvua mpaka maamuzi magumu ya wanakijiji kumvamia mganga huyo na kuumua.

‘’’sasa kuna nini jeshi la polisi kutowakamata waganga wa kienyeji wapiga ramli chonganishi Machimu Mwanandalo na Zingu Mwanazingula wakati hawa wapo katika kamati ya wazee waomba dua ya mvua pia ndiyo waliotuambia wananchi tuchange michango ya pesa,nafaka,nguo nyeusi au nyeupe kwa ajiri ya uombaji wa dua ya mvua’’’alisema ng’anghu

Hata hivyo wanakijiji hao walipaza sauti kwa ujumula ya kuwa wanahitaji kukamatwa kwa waganga hao ili kuwe na Imani na maafa yaliotokea 03/03/2015 saa 3:30 usiku kuwa ya mungu mwenyewe na  sio ya  kishirikina kama inavyosemekana kutokana  na mgogoro uliokuwepo mwanzo wa waganga wa kienyeji na wanakijiji kudai mvua walioichangisha michango.

Mwenyekiti wa kijiji cha mwakata Ezekial Saanane alivyohojiwa kuhusiana na maamuzi ya wanakijiji kuhitaji kukamatwa kwa waganga wa kienyeji wapiga ramli chonganishi alisema kwa sasa nipo katika harakati za kwenye majukumu ya kupokea wageni na watoa msaada hali hii ya wanakijiji kuchukua uamuzi huo ni kwa ajiri ya kupata jumuiko la kuweka  usahihi wa tukio la hivi karibuni.

‘’’Mvua ya mawe ilionyesha katika kijiji cha mwakata 03/03/2015 Saa 3:30 Usiku imereta Imani tofauti kati ya waganga na wazee wa kijiji hicho kufanya TAMBIKO la kuomba mvua ya kawaida waliokuwa wanaitaka inyeshe katika kijiji cha mwakata  na vijiji vingine na imekuja mvua isio na matarajio ya  kufanya uharibifu mkubwa wa mali,mazao,mifugo na nyumba kuharibika tuwe  wazi katika kuisemea serikali’’’alisema mwenyekiti.

Kamanda wa mkoa wa Shinyanga Justen Kamugisha alivyohojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na kuwakamata waganga wa kienyeji wapiga ramli chonganishi 2 alisema jambo hili la waganga wa jadi wapiga ramli chonganishi ni la utaratibu wa tulioupanga na kutolea maamuzi ya kisheria kutokana na mambo ya mauaji ya vikongwe,albino,mauaji ya kuchukua viungo vya binadamu.

Jambo la waganga wa kienyeji wa mwakata ambao wanakijiji wanataka tuwakamate na kuwafikisha katika vyombo vya sheria tunaomba watulie na waje katika ofisi zetu ilikupata uhakika wa Mwanandalo na Mwanazingula wanaotakiwa tuwakamate kwa utaratibu wa aina ipi wakati polisi ina utaratibu na maamuzi yake.

Aidha kamanda Kamugisha alisisitiza ya kuwa kuna utaratibu waganga wa kienyeji wanatakiwa waufuate na si vingine kamata kamata ya waganga wa kienyeji Inaendelea katika kata zote za mkoa wa Shinyanga ambapo tutatoa orodha ya yote ya waganga wa kienyeji wenye nyara za serikali,viungo vya binadamu na mauaji ya albino tutawapeleka mahakamani.

         ……………………..MWISHO…………………..

 

MWENYEKITI WA MTAA ALIYE SHITAKIWA KWA AJIRI YA MKOPO WA FEDHA



Obert  funga.

Kahama.

31/03/2015.

                                                     FEDHA  ZA  UCHAGUZI

Mwenyekiti  wa mtaa wa igalilimi kata ya kahama mjini wilayani hapa mkoani shinyanga, Bw,Ibrahimu Can Wally [CCM] ameshitakiwa mahakama ya mwanzo kwa kudaiwa fedha alizokopeshwa 12/06/2014 zilizodaiwa ni kwa ajiri ya kufanyia kapeni ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika 2014

Mfanyabiashara Bw,Sikujua Ndoi alimshitaki katika mahakama ya mwanzo kwa madai ya kumkopesha fedha zaidi ya Tshs milioni 4.5 kwa kufanya kampeni ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika 14/12/2014 na matokeo ya katoka akawa mshindi katika mtaa wa Igalilimi.

Awali mfanyabiashara Bw,Sikujua Ndoi alisema nimekuwa mpangaji wa chumba hiki zaidi ya miaka 10 kwa Bw,Ibrahim Cann amekuwa kama ndugu pia nimekuwa nikimwamini kwa ushirikiano wa kuheshimiana, Sasa alikuja hapa kunikopa  fedha ile heshima sikumnyima.

Nakumbuka  01/2/2013 alianza kuniambia kuhusiana na kumkopa fedha za kupigia kampeni za uchaguzi wa serikali za mtaa ilibidi tutafute watu wa heshima ili nimkabidhi kwa ushahidi wa kutosha,kweli jambo likafanyika kama tulivyoambizana tukapeana mbele ya watu 5

‘’’Barua kumb no,brz/10/3/02 iliotoka baraza la kata ya kahama mjini kwenda kwa  mfanyabiashara Sikujua Ndoi kwa kunishitaki  nitoke kwenye chumba 28/2/2015 bila sababu za msingi,barua hii ilinifanya nikimbilie mahakamani na kumfungulia kesi ya madai ya fedha zangu anilipe’’’alisema.

Kwa upande wa mwenyekiti wa mtaa ambaye pia ni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya [CCM] Bw,Ibrahimu wally canny alivyohojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na kukopa fedha kwa mfanyabiashara alisema mimi nachojua ni mpangaji wangu kama mambo ya mahakamani siwezi nikayasema jinsi yatakavyokuwa  na habari ya fedha kumkopa itajulikana mahakamani sina kauli zaidi ya hiyo.

 ‘’’’’  hata kama nilikopa mambo ya kumkopa  na mambo ya chumba ni tofauti na makubariano ya mkataba wa chumba,nataka aondokee tabia yake ni mbaya  tumefanya vikao vya mashitaka ya kumtuhumu ya kuwa yeye ni mwizi  kwenye maduka ya wenzie pia Natangaziwa vibaya katika mashitaka yangu ya nyumba ninakoishi wakati  wananchi wangu hawalijui yeye anaeneza mitaani’’’’alisema Ibrahim Canny

                 ………………MWISHO………………

Jumapili, 8 Machi 2015

Naobert funga.

WAATHIRIKA wa mvua ya mawe na upepo mkali iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 40 katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama, Shinyanga, jana walitawanywa kwa mabomu ya machozi na polisi wa kutuliza ghasia (FFU) baada ya kufunga barabara kuu ya Isaka-Kahama kuelekea nchi jirani za Rwanda, Uganda na Burundi, kwa kulala barabarani na kuweka mawe na miti.

Tukio hilo lililotokea aljajiri jana liliathiri baadhi ya wasafiri wa mabasi makubwa yaliyokuwa yakisafiri kwenda mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na mikoa ya jirani.

Waathirika hao walichukua uamuzi huo baada ya misaada ya chakula, magodoro, mablanketi na maturubai uliotolewa na wasamaria wema, ukiwa umefungiwa ndani ya darasa na wahusika wakishindwa kutimiza agizo la Waziri Mkuu Mizengo Pinda la kuwataka kuwapa msaada huo.

Akizungumza na Blogu hii, mwathirika wa tukio hilo, Benjamini Ndege, alisema wananchi waliamua kuchukua hatua hiyo ya kufunga barabara kutokana na kutojaliwa na serikali.

“Hawa waliofanya hivi ni wale ambao nyumba zao zimeharibika upande, zikiwa na mifugo na mali nyingine, lakini tunashindwa kuhudumiwa mahitaji muhimu…wanataka wote tukusanyike shuleni, sasa tunakaa hapo na mifugo yetu,” alihoji Ndege.

Ndege alisshangazwa na hatua ya mkuu wa wilaya ya Kahama, Benson Mpesya, kutumia polisi kuvurumisha mabomu wakati wakiwa katika majonzi ya kupoteza ndugu zao katika janga hilo.

Alisema mabomu yalirushwa na polisi hao, yamesababisha akinamama na watoto kukimbilia porini wakihofia maisha yao kutokana na kutowahi kuona hali hiyo.

Naye Salome Maganga wa kijiji cha Mwakata, alisema wanahitaji msaada walioahidiwa wapatiwe kwani hakuna wanachotegemeza zaidi ya serikali kuwatendea yale waliyowaahidi.

“Tumeahidiwa msaada mbalimbali, lakini hatupewi na mvua inanyesha tunabaki kulowa nje wakati maturubai yapo…tunaomba tufanyiwe yale aliyoahidi Waziri Mkuu,” alisema Maganga.

Alisema wameandamana na kufunga barabara kwa lengo la kuishinikiza serikali kuwapatia misaada husika.

DC MPESYA
Hata hivyo, licha ya vurugu hizo kudumu kwa saa moja na nusu, lakini waathirika hao walionekana kumkataa mkuu wa wilaya hiyo, Benson Mpesya kuwapo eneo hilo na kumtaka aondoke kutokana na kudaiwa kuamuru polisi kuwavurumishia mabomu.
 
Akizungumzia tukio hilo, Mpesya alisema vitendo vilivyofanywa vya kufunga barabara vilihamasishwa na viongozi wa kisiasa wanaonekana kuingilia mchakato wa ugawaji chakula cha msaada.
“Hii yote ni hawa viongozi wa kisiasa wanaoingilia mchakato huu, kama hawanitaki watafute njia nyingine na wala si kupitia hali hii ya msaada,” alisema Mpesya.

Mpesya alisema wananchi wote walioathirika na janga hilo, walipewa chakula cha siku tatu tangu juzi, na leo (jana), tunawapa magodoro, maturubai na mablanketi kupitia viongozi wao wa vijiji.
Alisema chakula tani 20 toka ghara kuu la chakula Shinyanga, kinatarajiwa kuwasili wakati wowote kutokana na agizo la Waziri Mkuu, Pinda.

OCD Kahama
Akizungumzia maandamano yaliyofanywa na waathirika hao, mkuu wa polisi wilaya ya Kahama, Leonard Nyandahu, alisema wanafuatilia ili kufahamu tatizo la wananchi hao kuandamana.

“Lazima wananchi watii sheria bila shuruti, hivi sasa kuna watu wanne tunawachunguza na pale watakapobainika tunawachukulia hatua za kisheria,” alisema OCD Nyandahu.

MBUNGE MAIGE
Naye mbunge wa jimbo la Msalala, Ezekiel Maige, alisema viongozi wa serikali wanashindwa kutimiza wajibu wao kwa waathirika hao na kuamua  kuwaangushia lawama wanasiasa.


“Wao ndiyo wanaozusha mgogoro huu, wananchi wanaambiwa na mkuu wa wilaya, chakula na vifaa vingine vipo vya kutosha, lakini hawavioni, sasa hapo nani wa kulaumiwa kama si wao…wanasiasa hawajeleta mvua hii lakini kikubwa ni kila mmoja kutimiza wajibu wake si kulaumiana,” alisema Maige.

Alisema kama misaada ipo kwa ajili yao, lazima viongozi wa serikali waitoe na kuwakabidhi wahusika wote waliokumbwa na janga hilo la mvua ya mawe na upepo mkali.


RC SHINYANGA
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Allynassoro Rufunga, alisema hali kwa waathirika wote inarejea kuwa vizuri kutokana na kukabidhiwa vifaa vyote husika vilivyotokana na msaada wa wasamaria wema.
 

Rufunga alisema serikali ya mkoa imetoa Sh.laki 3 kwa kila kaya kati ya 14 zilizofiwa kufuatia janga hilo lililotokea Jumanne usiku ikiwa ni rambirambi ili ziweze kuwasaidia kipindi hiki cha majonzi.

Alisema pesa hizo ni kati ya Sh.milioni 10 zilizotolewa na ofisi ya waziri mkuu ili kusaidia tukio hilo.

Hata hivyo, alisema misaada inayotolewa sasa kwa waathirika hao ni ile iliyotolewa na watu binafsi, taasisi zisizo za kiserikali na za kidini huku wakitakiwa kusubiri msaada wa serikali wakati wowote.

Aidha, Rufunga aliwaonya vijana wanaojiingiza kwa ajili ya kunufaika na misaada hiyo, kuacha mara moja tabia hiyo huku wakiwanyooshea kidole wananchi wa kijiji jirani cha Kagongwa kujiingiza katikati ya waathirika.

NAIBU WAZIRI AFYA
Akizungumza na baadhi ya waathirika wa janga hilo jana, Naibu waziri wa wizara ya afya, Kebwe Stephen, alisema wizara imetoa dawa zenye thamani ya Sh.milioni 47 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa janga hilo.
Kwa mujibu wa serikali, mvua hiyo ilisababisha vifo vya watu 42 na majeruhi 92

Jumatatu, 2 Machi 2015

BUSOKA NA KUCHELEWA



Na .OBERT FUNGA.

KAHAMA.

1/03/2015..                                                                               ELIMU                    

Wakazi wa kata ya busoka iliopo katika halmashauri ya mji wa kahama wilayani hapa,wameulalamikia uongozi wa wilaya  hiyo kwa kushindwa kuifungua shule ya secondari ya wasichana kata ya busoka ‘’baba haji busoka’’.

Wakazi hao walisema licha ya kukamilisha ujenzi  uliojengwa na kampuni  ya NIDA Textile Mills ambayo ilianza mchakato huo 2008/2009 na kukamilisha ujenzi wa shule hiyo 2010 ambayo ni kwa ajiri ya  wasichana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.

Mwaka 2011 kampuni ya NIDA ilikabidhi shule hiyo katika uongozi wa  halmashauri ya mji wa kahama zaidi ya miaka 6  iliopita mpaka sasa  haijafunguliwa bila sababu za msingi na imeshindwa kuifungua shule hiyo.

Kaimu meneja wa NIDA- Edson peter alisema  serikali na halmashauri ya mji wa kahama kuna jambo la sintofahamu kwa kushindwa kuendeleza  shule hiyo tulioikamilisha ujenzi uliogharimu kiasi cha Tshs,250 milion [CASH MONEY]

Peter aliongeza tumejitoa kimasomaso kukamilisha vyumba vya madarasa 15 yenye kila kitu kwa jinsi  ilivyokusudiwa tangu 2011 tulipoikabidhi halmashauri ya mji imeshindwa kuiendeleza na sasa imetelekezwa.

‘’’Kuna mambo ya siasa ambayo yanaingizwa kwenye elimu kutoka kwa mkuu wa wilaya ya kahama benson mpesya  ,,mbunge wa jimbo la kahama  james lembeli  na  wakuu wa idara ya  elimu,waratibu elimu kanda ya ziwa,ofisa elimu  wilaya  hii’’’alisema kwa masikitiko Peter

Baada ya kujenga shule hiyo mwekezaji aliomba iitwe  jina la baba haji busoka,kama kumbukumbu ya mtoaji wa misaada yenye tija katika wilaya ya kahama na nchini kwa ujumla.

Mkuu wa wilaya ya kahama benson mpesya alisema kutofunguliwa kwa wakati kwa  shule hiyo kuna sababu 2, mgodi wa bulyanhulu[acacia] kitengo cha miradi kimeyumba kutoa mahitaji muhimu,makubaliano  baina ya serikali ya wilaya  na mwekezaji yaliyumba kimpangokazi.

Mpesya alisema mgodi wa bulyanhulu[acacia]  uliingia makubaliano ya ujenzi  wa nyumba za walimu ili shule hiyo iweze kufunguliwa baada ya NIDA Tixtile Mills kujitolea  madarasa 15.

Makubaliano ya mgodi yalikuwa ni kusaidia vifaa vyote vya ujenzi  na halmashauri ya mji wa kahama itafute mkandarasi wa ujenzi ambapo wote 2 hawajakamilisha kusudio kamili.

Mpesya aliongeza ya kuwa meneja miradi wa mgodi wa bulyanhulu Giten Givecha ameshinwa kuonyesha ushirikiano kwa kukamilisha ujenzi wa nyumba za walimu na vifaa vingine.

Kwa upande wa mkurungenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa kahama Felix kimaryo alisema  itafunguliwa iwapo ofisi ya elimu kanda ya ziwa kufanya ukaguuzi na mambo yote yatakuwa kamilifu shule hiyo itaanza kutumika  ‘’’ miaka sita  haijakamilika……NI   lini   Itakamilika??????’’’.

                    …………..MWISHO…………..

USHETU;



Obert  funga.

Kahama.

2/03/2015

Mjumbe wa kamati kuu taifa katika halmashauri ya mji wa kahama wilayani kahama mkoani shinyanga Sebastiani Tobias [komaa] amewatahadharisha wenyeviti wa mtaa wa nyihogo na mtaa wa sazia ya kuwa wawe makini kwa fitina za ccm.

 Akiwahutubia wananchi katika hafla iliofanyikika katika viwanja vya nyihogo soko la miwa bw, sebastiani alisema tumefanya hafla ya kuwashukru wenyeviti wa mitaa kutokana na mateso ya ccm  tukiwa katika hali mbaya ya wizi,dhuluma,manyanyaso na kubezwa.

‘’bado miezi michache ya kuingia kwenye harakati za uchaguzi fitina za ccm kuwe na umakini  wa kufanya harakati za maendeleo na vita ya vyama bila ya kuwa na jitihada za ziada kutakuwa na mchezo mchafu’’alisema.

Sebastini aliongeza Chadema imejipanga vyema katika uchaguzi mkuu wa mwezi 10 kwa matokeo ya kufurahika, tutaanza  kutazama  daftari la wapiga kula,vitambulisho vya kupigia kula na maandalizi  yatakayo tulidhisha bila hivyo kitaeleweka mpaka chadema iwe na uhuru.

Aidha mwenyekiti wa chadema wilaya ya kahama juma protas ntahipera alisema mwezi wa 2 watampeleka mahakamani  aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa wa majengo bw,mseveni mukula kwa dhuluma ya fedha za michango na kujichukulia maeneo ya ardhi.

Hata hivyo hafla hiyo ilivulugika mara baada ya kuja vijana wa mitaani kwa kunyang’anya chakula kwa akinamama wapishi ikiwemo kamati ya maandalizi kushindwa kuithibiti vulugu ya vijana hao licha ya kuwa na brigedi 10 [askari] wa chama cha chadema.

Mpaka muda wa 12:48 jioni chakula kilichopikwa ni  sufuria 7 za chakula sufuria 3 za nyama, kilikuwa kimeliwa na vijana zaidi ya 140 na kubakiwa na sufuria 1 la wali ambalo wapishi walisusa kula walitaka walipwe pesa ya upishi.

                              ……………Mwisho…………..