Jumatatu, 2 Machi 2015

WATOTO MITAANI NA VIJANA WAJASILIAMALI



Obert  funga.

Kahama.

01/03/2015.                                              WATOTO

Halmashauri ya mji wa kahama wilayani hapa,imetakiwa kuwakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na mazingira magumu waliopo katika standi za basi,majumba yasio kamilika warudishwe makwao.

Wito huo ulitolewa jana katika sherehe ya tathimini ya 2014 na katibu wa umoja wa wazee kahama UWAKA paul nkwabi alisema watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kipindi hiki cha masika ni kibaya kwa magojwa.

Nkwabi alisema watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ni zaidi ya 106 kwa takwimu za taasisi za utetezi wa haki za binadamu SHIHABI,TALEIN na care Intenational pia hata kituo cha mvumwa kilichopo kata ya nyahanga.

‘’serikali isitafute lawama kwa UWAKA wakati haifanyi wajibu unaostahiki mpaka tuwe tunawaambia kila jambo watoto hao wanalala kwenye vibaraza vya maduka,kwenye majumba mabovu,kwenye mitalo na sehemu za hatari.

Kwa upande wa mwenyekiti wa CCM mkoa wa shinyanga Khamisi mgeja ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo alisema naunga mkono kwa 100% jambo hili lifanyiwe uharaka kwa kuwarudisha makwao watoto hao.

Wanahangaika watoto hawa kwa njaa,maradhi,malezi na sehemu ya kulala, serikali ifanye mchakato wa haraka ikisaidiana na taasisi za haki za binadamu,dawati la jinsia,vituo vya kulelea watoto na mashirika mengineyo.

Mkurugenzi mtendaji wa mji felix kimaryo alisema jambo hili la kuwarudisha watoto linafanyika na litakuwa endelevu mpaka mwezi wa 21/3/2015 na tutatoa takwimu halisia ya watoto waliorudishwa na waliobaki.

                     …………MWISHO…………

Obert  funga.

Kahama.

01/03/2015.                                           VIJANA

Kikundi cha ujasilimali cha vijana na maendeleo kilichopo katika kata ya nyihogo wilayani kahama mkoani shinyanga,wamepewa mchango wa kuku 500 na wakili nkuba kwa kukijenga na kukiendeleza kikundi hicho kwa hali ya upendo.

Hali hiyo ilijitokeza jana kwenye sherehe ya kikundi cha vijana na maendeleo ambapo mgeni rasmi wa kikundi hicho alikuwa Wakili Nkuba ambaye aliambatana na katibu wa mbunge wa jimbo la kahama Abdul  Ntahokaja.

Awali kikundi cha vijana na maendeleo kilisoma risala kwa mgeni rasmi na wageni walikwa kwa mapungufu na changamoto  za mahitaji na malengo makubwa ya kukamilisha kikundi ili kiwezekukidhi mradi kusudiwa.

Mwenyekiti wa kikundi cha vijana na maendeleo Yohana Jackson aliyesoma risala alisema tumebuni mradi wa ufugaji wa kuku licha ya kujishughulisha na ajira za photo copy,ushonaji vitambaa,biashara ndogondogo na kukopeshana mchango.

Mgeni rasmi aliahidi kutoa kuku 500 endapo ujenzi wa banda utakapo kamilika na kuwapa ushauri wa kujiandaa na maandalizi ya ufugaji wa kuku kwa magonjwa,ajali,kung’atwa na nyoka,lishe,pahala safi na huduma stahiki.

Naye katibu wa mbunge abdul ntahokaja alisema nimetumwa na mbunge james lembeli kuwakilisha kiasi cha fedha Tsh,1000,000 kama mchango wa kikundi cha vijana na maendeleo  kilicho mwandikia barua ya kumkaribisha ashiriki katika sherehe ya ufunguzi.

Aidha ntahokaja alisema mbunge amekwenda arusha kwa shughuli za kitaifa lakini ameona hawezi kuacha kufika ndiyo maana nimefika mimi badala yake pia hakijaharibika kitu,fedha za mchango wa vijana wanaojituma,kujiajiri na kuweka ujasiliamali kwa kujiamini zipo.

                             ………….MWISHO……………

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni