Jumatatu, 2 Machi 2015

USHETU;



Obert  funga.

Kahama.

2/03/2015

Mjumbe wa kamati kuu taifa katika halmashauri ya mji wa kahama wilayani kahama mkoani shinyanga Sebastiani Tobias [komaa] amewatahadharisha wenyeviti wa mtaa wa nyihogo na mtaa wa sazia ya kuwa wawe makini kwa fitina za ccm.

 Akiwahutubia wananchi katika hafla iliofanyikika katika viwanja vya nyihogo soko la miwa bw, sebastiani alisema tumefanya hafla ya kuwashukru wenyeviti wa mitaa kutokana na mateso ya ccm  tukiwa katika hali mbaya ya wizi,dhuluma,manyanyaso na kubezwa.

‘’bado miezi michache ya kuingia kwenye harakati za uchaguzi fitina za ccm kuwe na umakini  wa kufanya harakati za maendeleo na vita ya vyama bila ya kuwa na jitihada za ziada kutakuwa na mchezo mchafu’’alisema.

Sebastini aliongeza Chadema imejipanga vyema katika uchaguzi mkuu wa mwezi 10 kwa matokeo ya kufurahika, tutaanza  kutazama  daftari la wapiga kula,vitambulisho vya kupigia kula na maandalizi  yatakayo tulidhisha bila hivyo kitaeleweka mpaka chadema iwe na uhuru.

Aidha mwenyekiti wa chadema wilaya ya kahama juma protas ntahipera alisema mwezi wa 2 watampeleka mahakamani  aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa wa majengo bw,mseveni mukula kwa dhuluma ya fedha za michango na kujichukulia maeneo ya ardhi.

Hata hivyo hafla hiyo ilivulugika mara baada ya kuja vijana wa mitaani kwa kunyang’anya chakula kwa akinamama wapishi ikiwemo kamati ya maandalizi kushindwa kuithibiti vulugu ya vijana hao licha ya kuwa na brigedi 10 [askari] wa chama cha chadema.

Mpaka muda wa 12:48 jioni chakula kilichopikwa ni  sufuria 7 za chakula sufuria 3 za nyama, kilikuwa kimeliwa na vijana zaidi ya 140 na kubakiwa na sufuria 1 la wali ambalo wapishi walisusa kula walitaka walipwe pesa ya upishi.

                              ……………Mwisho…………..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni