NGUMI 1
Na .Obert funga.
Kahama.
2/03/2015. VURUGU CCM
Wakati homa ya uchanguzi
mkuu wa rais,wabunge,madiwani ikiwa inaanza kupanda,viongozi wa [CCM] na umoja
wa wzee kahama UWAKA kata ya malunga wilaya ya kahama mkoani shinyanga wameanza
mgogoro wa kutuhumiana.
Akizungumza na waandishi wa
habari mwenyekiti wa CCM kata ya malunga Donard Iguru alisema chanzo cha
kunyosheana vidole na umoja wa wazee kata ya malunga [UWAKA-Kata] na kukaa
vikao viwili vya usululishi ambapo bado maneno yanatokea ya uongozi wa kata
kuto waheshimu wazee.
Awali kipindi cha uchaguzi
wa serikali za mitaa wazee wa [uwaka] john ngassa na phil lugwalalira waliingilia madaraka ya uongozi wa CCM kata ya malunga
kwa kuwachagulia wenyeviti waliokuwa wakigombea mitaa wanaotoka [chadema] bila kuiweka ccm
katika orodha nzuri.
Iguru aliongeza ya kuwa John
ngassa yeye ni chadema anatuchagulia vijana wake wa chadema na kutulazimisha
tuwasimamishe kugombea uongozi wakati ccm tunajiweza anatuambia yeye kama mzee
wa UWAKA anamaamuzi ya kutuambia jambo la chama bia kufuata sheria na sera za
chama .
CCM iliwachagua vijana
wanaofaa kwa uongozi wa serikali ya mtaa lakini tumeshinda mtaa wa korogwe mwenyeviti
Edward makomba kati mitaa 3 ya Igomelo na malunga ambayo tumenyang’anywa na chama
cha upinzani.
Baada ya matokeo ya uchaguzi yalioanza
14/12/2014 kulitokea kutoelewana‘’tulifanya kikao cha kuombeana msamaha’’Tuliwaarika
mwenyekiti wa UWAKA wa wilaya ya kahama Mashaka kilonda pia upande wa CCM
Tulimuomba aje katibu mwenezi wilaya bw, Masud Merimeri lakini wazee walimkataa
masud merimeri.
Wazee hao walifanya kikao na
watu hao binafsi cha kumzodoa mwenyekiti wa mtaa korogwe Edward makomba CCM wakahamia
kwa katibu mwenezi wilaya masud merimeri
ya kuwa ni mla rushwa wa tozo za ushuru wa Jengo la CCM wilaya.
Hata hivyo wazee hao ambao hawajui kanuni na
sheria zilizopo katika katiba ya UWAKA,pia CCM kwa fedha za wapangaji wa vyumba
wazee hao walisema TAKUKURU hawakumchunguza vyema masud merimeri 2013/2014
wakati sakata lilikuwa la kumtia hatiani.alisema Iguru
Mwenyekiti wa umoja wa wzee kahama[UWAKA]-
Mashaka kilonda alisema viongozi wa CCM malunga kusigana na wazee wa uwaka ni
uroho wa madaraka na tamaa isiokuwa na ubusara kwa kufanyiana umangimeza usio
na tija ya kisiasa.
………..MWISHO………
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni