Jumatatu, 2 Machi 2015

BUSOKA NA KUCHELEWA



Na .OBERT FUNGA.

KAHAMA.

1/03/2015..                                                                               ELIMU                    

Wakazi wa kata ya busoka iliopo katika halmashauri ya mji wa kahama wilayani hapa,wameulalamikia uongozi wa wilaya  hiyo kwa kushindwa kuifungua shule ya secondari ya wasichana kata ya busoka ‘’baba haji busoka’’.

Wakazi hao walisema licha ya kukamilisha ujenzi  uliojengwa na kampuni  ya NIDA Textile Mills ambayo ilianza mchakato huo 2008/2009 na kukamilisha ujenzi wa shule hiyo 2010 ambayo ni kwa ajiri ya  wasichana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.

Mwaka 2011 kampuni ya NIDA ilikabidhi shule hiyo katika uongozi wa  halmashauri ya mji wa kahama zaidi ya miaka 6  iliopita mpaka sasa  haijafunguliwa bila sababu za msingi na imeshindwa kuifungua shule hiyo.

Kaimu meneja wa NIDA- Edson peter alisema  serikali na halmashauri ya mji wa kahama kuna jambo la sintofahamu kwa kushindwa kuendeleza  shule hiyo tulioikamilisha ujenzi uliogharimu kiasi cha Tshs,250 milion [CASH MONEY]

Peter aliongeza tumejitoa kimasomaso kukamilisha vyumba vya madarasa 15 yenye kila kitu kwa jinsi  ilivyokusudiwa tangu 2011 tulipoikabidhi halmashauri ya mji imeshindwa kuiendeleza na sasa imetelekezwa.

‘’’Kuna mambo ya siasa ambayo yanaingizwa kwenye elimu kutoka kwa mkuu wa wilaya ya kahama benson mpesya  ,,mbunge wa jimbo la kahama  james lembeli  na  wakuu wa idara ya  elimu,waratibu elimu kanda ya ziwa,ofisa elimu  wilaya  hii’’’alisema kwa masikitiko Peter

Baada ya kujenga shule hiyo mwekezaji aliomba iitwe  jina la baba haji busoka,kama kumbukumbu ya mtoaji wa misaada yenye tija katika wilaya ya kahama na nchini kwa ujumla.

Mkuu wa wilaya ya kahama benson mpesya alisema kutofunguliwa kwa wakati kwa  shule hiyo kuna sababu 2, mgodi wa bulyanhulu[acacia] kitengo cha miradi kimeyumba kutoa mahitaji muhimu,makubaliano  baina ya serikali ya wilaya  na mwekezaji yaliyumba kimpangokazi.

Mpesya alisema mgodi wa bulyanhulu[acacia]  uliingia makubaliano ya ujenzi  wa nyumba za walimu ili shule hiyo iweze kufunguliwa baada ya NIDA Tixtile Mills kujitolea  madarasa 15.

Makubaliano ya mgodi yalikuwa ni kusaidia vifaa vyote vya ujenzi  na halmashauri ya mji wa kahama itafute mkandarasi wa ujenzi ambapo wote 2 hawajakamilisha kusudio kamili.

Mpesya aliongeza ya kuwa meneja miradi wa mgodi wa bulyanhulu Giten Givecha ameshinwa kuonyesha ushirikiano kwa kukamilisha ujenzi wa nyumba za walimu na vifaa vingine.

Kwa upande wa mkurungenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa kahama Felix kimaryo alisema  itafunguliwa iwapo ofisi ya elimu kanda ya ziwa kufanya ukaguuzi na mambo yote yatakuwa kamilifu shule hiyo itaanza kutumika  ‘’’ miaka sita  haijakamilika……NI   lini   Itakamilika??????’’’.

                    …………..MWISHO…………..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni