Jumatatu, 2 Machi 2015

mwenyekiti wa mtaa ashitakiwa kwa madeni



Obert  funga.

  Kahama.

  28/02/2015.                                                     FEDHA  ZA  UCHAGUZI

Mwenyekiti  wa mtaa wa igalilimi kata ya kahama mjini wilayani hapa mkoani shinyanga, Bw,Ibrahimu Can Wally [CCM] ameshitakiwa mahakama ya mwanzo kwa kudaiwa fedha alizokopeshwa 12/06/2014 zilizodaiwa ni kwa ajiri ya kufanyia kapeni ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika 2014.

Mfanyabiashara Bw,Sikujua Ndoi alimshitaki katika mahakama ya mwanzo kwa madai ya kumkopesha fedha zaidi ya Tshs milioni 4.5 kwa kufanya kampeni ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika 14/12/2014 na matokeo yakatoka akawa mshindi katika mtaa wa Igalilimi.

Awali mfanyabiashara Bw,Sikujua Ndoi alisema nimekuwa mpangaji wa chumba hiki zaidi ya miaka 10 kwa Bw,Ibrahim Cann amekuwa kama ndugu pia nimekuwa nikimwamini kwa ushirikiano wa kuheshimiana, Sasa alikuja hapa kunikopa  fedha ile heshima sikumnyima.

Nakumbuka  01/2/2013 alianza kuniambia kuhusiana na kumkopa fedha za kupigia kampeni za uchaguzi wa serikali za mtaa ilibidi tutafute watu wa heshima ili nimkabidhi kwa ushahidi wa kutosha,kweli jambo likafanyika kama tulivyoambizana tukapeana mbele ya watu 5.

‘’’Barua kumb no,brz/10/3/02 iliotoka baraza la kata ya kahama mjini kwenda kwa  mfanyabiashara Sikujua Ndoi kwa kunishitaki  nitoke kwenye chumba 28/2/2015 bila sababu za msingi,barua hii ilinifanya nikimbilie mahakamani na kumfungulia kesi ya madai ya fedha zangu anilipe’’’alisema.

Kwa upande wa mwenyekiti wa mtaa ambaye pia ni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya [CCM] Bw,Ibrahimu wally canny alivyohojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na kukopa fedha kwa mfanyabiashara alisema mimi nachojua ni mpangaji wangu kama mambo ya mahakamani siwezi nikayasema jinsi yatakavyokuwa  na habari ya fedha kumkopa itajulikana mahakamani sina kauli zaidi ya hiyo.

                 ………………MWISHO………………

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni