Jumatatu, 2 Machi 2015

LEMBELI NA NGUO



Obert funga.

Kahama.

2/03/2015.                              SOSOPI   asema  Bavicha

Chama cha demokrasia na maendeleo ‘Chadema’wilayani kahama mkoani Shinyanga,kimemtaka  mbunge wa jimbo la kahama Bw,James Lembeli ajiweke kwenye msimamo wa kujionyesha  kutokana na maamuzi yake ya kukataa kila jambo linalotokea ndani ya ccm.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika kata ya nyihogo katika viwanja vya Bwawani makamu mwenyekiti wa [Bavicha]Bw,Patrick Ole Sosopi alisema harakati za Samweli Sitta,James Lembeli na harrson mwakyembe ilikuwa na ajenda kwa watanzania lakini imezimwa kwa kufanyiana hujuma ilioanza kwa mwakyembe.

Bw,Sosopi aliongeza ya kuwa Lembeli amekuwa ccm kwa bahati mbaya toka awali alikuwa na majibu ya kuwa tofauti na malengo ya ccm ndiyo maana hakuna Utekelezaji wa kauli ya Rais aliosema akaikubali.

Kamati ya maadili ya ccm ilimtishia kumnyang’anya kadi alijibu ‘’ccm sio mama yangu’’sakata la Uwaziri wa maige alipiga msumari mkali,tokomeza ujagili wana ccm kawamwaga,katiba ya jaji walioba,escrow na kuwekwa kiporo kwa peter mhongo vyote kamkana Rais kaikana ccm.

‘’’imekuwa kawaida kwa mbunge wa jimbo la kahama na mbunge wa jimbo la msalala kuungana na hoja za chadema zikitolewa bungeni zaidi ya miaka yote waliokuwa wana ungamkono kwa 100%’’’alisema

Aidha Bw,Sosopi alisisitiza kwa kuwaambia wananchi ya kuwa viongozi wote waliokwenda loliondo kwa babu Ambilikile mwasapile kunywa dawa ndiyo wenye kuto tekeleza wajibu wa maendeleo kama mbunge Lembeli ambaye jimbo la kahama hakuna kumbukumbu zaidi ya saccos 3.

 Licha ya kutumia mfuko wa jimbo kwa miradi mbalimbali kwa kuchangia shule,kikundi,zahanati,nyumba za walimu na ofisi mbalimbali lakini hakuna majibu ya Uhakika ya matekelezo kutokana na eneo husika kuwa vilevile kama alivyolikuta na hakuna afisa mtendaji aliye mshitaki.

Tunataka Lembeli afanye mrejesho wa kila pahala alipotoa mchango wa mfuko wa jimbo atoe majibu kama halmashauri ya ushetu kuna kata 6 zimechukua michango lakini hakuna matekelezo pia halmashauri ya mji kuna kata 7 hakuna utekelezaji.

                ………………..MWISHO…………………. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni