Jumatatu, 2 Machi 2015

mwalimu wa shule ya msingi kinamapula



Obert  funga.

Kahama.

2/03/2015.                                                  MWALIMU  AKIMBIA  TUKIO

Mwalimu wa shule ya msingi kinamapula Burugu Kayagira[wakujitolea] iliopo kata ya kinamapula katika halmashauri ya ushetu wilayani kahama mkoani shinyanga,amekimbia katika eneo la kazi mara baada ya kuwadhibu wanafunzi wa darasa la saba.

Wanafunzi waliojeruhiwa vidoleni ni 3 na waliojeluhiwa maeneo mbalimbali ni 3 kwa kukaidi amri ya mwalimu huyo ya kuwalazimisha kuzoa kinyesi kwa mikono wanafunzi hao wakishirikiana na mwalimu wa zamu zuhura mboja.

Hata hivyo wazazi wakilieleza gazeti hili ya kuwa wanafunzi waliopigwa  viboko zaidi ni wanafunzi 6 kuliko wengine ambao walikubali kushika kwa mikono bila kutumia kifaa cha aina yeyote.

Awali 19,02,2015 muda wa asubuhi katika shule hiyo kulitokea tukio la kuona vinyesi vingi vya watu wakubwa katika darasa la saba ambavyo vilionekana ni ushirikina uliopo katika shule hiyo.

Mwalimu Burugu Kayagira aliwaadhibu wanafunzi hao kwa kutotii amri yake aliowaelekeza ya kuzoa kwa mikono vinyesi hivyo ndipo alianza adhabu ya kuwapiga kwa mfululizo wa viboko maeneo mbalimbali na kusababisha wanafunzi 3 kuumia vibaya na wengine 3 kuumia mikononi.

Mwenyekiti wa shule ya msingi ya kinamapula Bw,Elias Kachembe aliliambia gazeti hili ya kuwa turifanya kikao cha dharula kwa ajiri ya mgogoro huu lakini wazazi walikuwa na dhamira ya kumshitaki huyu mwalimu ndipo alikimbia mpaka sasa hatujui alipokimbilia.

’’’jambo la kuwalazimisha  halikuwepo isipokuwa adhabu ya viboko ndiyo iliomgharimu kwa kuwapiga kiasi cha kuumia lakini nao wazazi wanakuja mbiombio kufanya ugomvi bila busara ya kumwita mwalimu mkuu au mimi tukae kwa kujadili kilicho tokea’’’alisema.

Mwalimu mkuu Vumilia Ndessi alitafutwa kwa njia ya simu-kujibu yaliotokea shuleni kwake alikiri ya kuwa kweli kulitokea adhabu ya namna hiyo lakini mwalimu burugu kayagira aliyekuwa kwenye kipindi cha asubuhi darasa la saba amekimbia bado ajaripoti ofisini.

Kaimu afisa elimu msingi wilayani hapa Bw,Silvanus Bonda alisema ni mara ya pili shule hii kuletewa malalamiko ya kuhusiana na walimu,wanafunzi kuteswa,kamati ya shule kutofuata utaratibu  uliopagwa na mihtasari ya ajenda kuikamilisha kama lengo la mikakati.

‘’’jambo hili litakuwa limenizidi uwezo wangu mpaka viongozi wa juu maana hao ndiyo litakamilika kwa kuona wapi pana ulegevu kutoka ya 2014 na ya sasa 2015 kufuatana na mihtasari ya vikao na taarifa iliofika kwenye ofisi ya mkurugenzi’’’alisema.

Aidha kaimu afisa elimu alisema kuna jambo lenye utata kwa mikakati ya juhudi ya kulimaliza ‘gogoro’ la aina hii bado kuliweka sawa kwa vile hatujakutana tulijue mwanzo na mpaka kufika lilipo tutalifanyia kazi baada ya kukaa kikao cha pamoja.

       …………MWISHO………….

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni