WAGANGA WANAO ANDAMWA NA WANANCHI
Obert funga.
Kahama.
31/03/2015. Waganga wa kienyeji
Wakazi wa kijiji cha mwakata na Igugunwa katika kata ya Isaka wilayani hapa mkoani
shinyanga wamewalalamikia jeshi la polisi kwa azma ya kuwakamata waganga wa
kienyeji wapiga ramli chonganishi huku wakiachwa waganga wa kienyeji 2 bila
sababu yeyote.
licha ya serikali na wahisani mbalimbali kutoa misaada ya
pesa,vifaa,vyombo na ujenzi wa nyumba za haraka kwa waadhirika wa majanga ya
mvua ya mawe ilioikumba kijiji cha mwakata na Igugunwa kuua wananchi 48 na
majeruhi 118 huku ikiwaacha wakazi 512 wakiwa hawana pa kuishi mpaka sasa
utaratibu unafanyika wa kuwajengea eneo lenye maakazi.
Makizungumza kwa nyakati tofauti katika kijiji hicho walisema
tupo katika kuweka jambo hili kwenye tahadhari ya waganga wa kienyeji
waliosalia kwa mtafaluko uliokuwepo mwanzo kwa madai ya michango ya dua ya mvua
iliochangishwa na waganga 2 kati ya kamati ya wazee 19 alisema Sofia Shija
mkazi wa mwakata.
Awali kulikuwa na michango ya kamati ya wazee waomba dua
ya mvua tokea 23/01/2015 ambayo kamati ina wazee 19 iliotufanya tuchange
michango mbalimbali zaidi ya mara 3 kwa wachangishaji waliotuletea tangazo la
kikao cha dua ya mvua.alisema Bi,Sofia
Naye Shabani ng’anghu mkazi wa kijiji hicho alisema
hasira ya mganga wa kienyeji [mwanamaria]aliyeuawa na wanakijiji kwa kutoongea
ukweli wa jambo la kuchangisha michango ya mvua mpaka maamuzi magumu ya
wanakijiji kumvamia mganga huyo na kuumua.
‘’’sasa kuna nini jeshi la polisi kutowakamata waganga wa
kienyeji wapiga ramli chonganishi Machimu Mwanandalo na Zingu Mwanazingula
wakati hawa wapo katika kamati ya wazee waomba dua ya mvua pia ndiyo
waliotuambia wananchi tuchange michango ya pesa,nafaka,nguo nyeusi au nyeupe
kwa ajiri ya uombaji wa dua ya mvua’’’alisema ng’anghu
Hata hivyo wanakijiji hao walipaza sauti kwa ujumula ya
kuwa wanahitaji kukamatwa kwa waganga hao ili kuwe na Imani na maafa yaliotokea
03/03/2015 saa 3:30 usiku kuwa ya mungu mwenyewe na sio ya
kishirikina kama inavyosemekana kutokana
na mgogoro uliokuwepo mwanzo wa waganga wa kienyeji na wanakijiji kudai
mvua walioichangisha michango.
Mwenyekiti wa kijiji cha mwakata Ezekial Saanane
alivyohojiwa kuhusiana na maamuzi ya wanakijiji kuhitaji kukamatwa kwa waganga
wa kienyeji wapiga ramli chonganishi alisema kwa sasa nipo katika harakati za
kwenye majukumu ya kupokea wageni na watoa msaada hali hii ya wanakijiji
kuchukua uamuzi huo ni kwa ajiri ya kupata jumuiko la kuweka usahihi wa tukio la hivi karibuni.
‘’’Mvua ya mawe ilionyesha katika kijiji cha mwakata
03/03/2015 Saa 3:30 Usiku imereta Imani tofauti kati ya waganga na wazee wa
kijiji hicho kufanya TAMBIKO la kuomba mvua ya kawaida waliokuwa wanaitaka
inyeshe katika kijiji cha mwakata na
vijiji vingine na imekuja mvua isio na matarajio ya kufanya uharibifu mkubwa wa mali,mazao,mifugo
na nyumba kuharibika tuwe wazi katika
kuisemea serikali’’’alisema mwenyekiti.
Kamanda wa mkoa wa Shinyanga Justen Kamugisha alivyohojiwa
na waandishi wa habari kuhusiana na kuwakamata waganga wa kienyeji wapiga ramli
chonganishi 2 alisema jambo hili la waganga wa jadi wapiga ramli chonganishi ni
la utaratibu wa tulioupanga na kutolea maamuzi ya kisheria kutokana na mambo ya
mauaji ya vikongwe,albino,mauaji ya kuchukua viungo vya binadamu.
Jambo la waganga wa kienyeji wa mwakata ambao wanakijiji
wanataka tuwakamate na kuwafikisha katika vyombo vya sheria tunaomba watulie na
waje katika ofisi zetu ilikupata uhakika wa Mwanandalo na Mwanazingula
wanaotakiwa tuwakamate kwa utaratibu wa aina ipi wakati polisi ina utaratibu na
maamuzi yake.
Aidha kamanda Kamugisha alisisitiza ya kuwa kuna
utaratibu waganga wa kienyeji wanatakiwa waufuate na si vingine kamata kamata
ya waganga wa kienyeji Inaendelea katika kata zote za mkoa wa Shinyanga ambapo
tutatoa orodha ya yote ya waganga wa kienyeji wenye nyara za serikali,viungo
vya binadamu na mauaji ya albino tutawapeleka mahakamani.
……………………..MWISHO…………………..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni