Obert
funga.
kahama.
9/4/2015
.tuhumaya Katekista
Kanisa katoriki parokia ya Mt.Kalori Lwanga
jimbo la katoriki kahama katika kata ya kahama mjini wilayani hapa mkoani
shinyanga, limeingia tena kwenye kashfa ya michango holela ilioanza 2012-2015
inayochangishwa na Kateksta Samson magoke bila uongozi wa jimbo kulitambua.
Waumini wa kanisa katorikIi mt.karoli lwanga
jimbo la kahama wakizungumza na waandishi wa habari walisema tumekuwa na
mgogoro na Kateksta Magoke kwa fedha
za michango ya wapiga picha
wanazotozwa waingiapo kanisani kupiga picha
za matukio ya Sakramenti,Ubatizo,Misa
mbalimbali hatoi jibu la
kueleweka kwa kuwaeleza
waumini zinafanya kazi gani? Zipo
kigango kipi? Au benki ipi? Zimefikia kiasi
gani ? pia kitabu cha risti kimeandikwaje?
.
Naye Joshua Antoni alisema Kateksta huyu
amekuwa ombaomba kwa fedha za aina
mbalimbali kwetu hata mihuri na risti zitolewazo kwenye kitabu cha risti
tofauti na mlengo wa kanisani batili hatutambui zinafanya shughuli ipi? Na zipo kwenye kitengo
gani? Pia hazina Baraka kwa Mapadri wote,Baba Paroko
na Askofu Rodriki Minje.
2008-2009 kanisa katoriki jimboni hapo
lilipata kashfa ya Kateksta
selestan Amubi kufumaniwa na mwanamke wa Kinyarwanda Ngirwa Kamkara‘21’wakiwa hana
nguo saa 5:45 jioni katika kata ya Majengo guest ya Mayunga B ambapo mwanamke huyo
alikimbia na nguo za Katekista
huyo.
Mwenyekiti wa
umoja wa wapiga picha wilaya
ya kahama ‘’UWAPIKA’’Charles Richard shinwa akizungumza na waandishi wa
habari jimboni hapo alisema tumekuwa
tunabaguliwa na kutozwa shs,5000 kwa
kila mpiga picha za kawaida mmoja,mchukua video shs,10,000-12,000 na
baisikeli shs.700,pikipiki shs.1500 toka 2013-2014.
Bw,Shinwa
alisisitiza jambo hili la Katekista kufanya
Ubaguzi kwa baadhi ya wapiga picha waingipo na kutozwa na
wapo wasiotozwa kuna waaumini ambao
wanasari hapahapa mpaka sasa nao
wanatozwa kiwango cha shs.4000 wengine hawatozwi hicho ndicho
kilicholeta mtafaruku kati ya
Katekista Samson Magoke na wadada wawili wanaoshirikiana naye
wametuletea vitambulisho batili na risti zenye mhuri Usiotambulika.
‘’Tumewekewa mistari miwili ya waaumini
kupita ili wapigwe picha inatuchanganya wakati wa kupiga picha maana mhusika
anakuwa upande mwingine
na sisi wapiga picha tupo upande mwingine huku tumelipishwa fedha na kuwekewa masharti ya kupewa kitambulisho mwisho wa shughuli tunawarudishia
kitambulisho ambacho hakina mhuri
unaotambulisha ipasavyo’’.alisema Bw,Shinwa.
Waandishi wa habari walivyomtafuta Katekista
Samson Magoke ili atoe ufafanuzi wa tozo za wapiga picha na waumini wanaopiga
picha alisema fedha zinazotozwa ni kusaidia wanaofanya usafi wa ndani na nje ya
kanisa hili licha ya kutotangaza ila ni utaratibu wa
kwetu sisi viongozi tulioweka kuanzia
2012-13 hatukuwashirikisha Mapadri,Baba
Paroko na Askofu Rodrck
Minje.
Baba paroko jimbo la katoriki kahama
Robert Lujura alisema sina taarifa ya aina hiyo nitafanya kikao na
katibu wa jimbo,Katekista huyo kwa maelezo
ya ufasaha kwa jambo hili lenye
Uchuuzi wa waaumini na wapiga picha waingiao
kanisani bila kuwatangaziwa waumini
na wapiga picha kama kutakuwa na
utaratibu wa kuwatoza fedha za kuingia kanisani
ikiwa na baiskeli na
pikipiki.
‘’Hili
jambo ni la ajabu na
aibu kwa Katekista kujifanyia maamuzi yenye muono
wa kibinafsi pasipo
kufuata neno la mungu na
utaratibu wa kanisa katoliki
ulivyo na unavyofanya kwa nyakati hizi za ufufuo wa yesu kwa
kiongozi wa kanisa kafanya makosa makubwa kwa makusudi ya
uroho wa tamaaya fedha’’alisema Baba Paroko.
Upande wa Askofu Rodrick Minje alivyotafutwa
na waandishi wa habari kwa njia ya
simu haikupatikana ili kupata
ufafanuzi wa michango inayotozwa
kanisani kwa utaratibu wa Katekista Samsoni Magoke aliokuwa nao tangu 2012-13 mpaka sasa anaendelea kuwatoza waumini na
wasiokuwa waumini kwa kiwango
kikubwa.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni