MREMBO AFARIKI BAADA YA KUBUGIA DAWA ZA KUPUNGUZA UNENE,
Ni
binti mrembo wa miaka 21 aliyefikia Chuoni kimasomo ambapo alichukua
maamuzi ya kununua dawa za kupunguza/kujikinga na unene alizozinunua
kwenye mtandao (online).
April 12 2015 ndio ilikua siku yake ya
mwisho duniani baada ya kulazwa hospitali na chanzo cha kifo chake
kikiaminika ni hivyo vidonge ambavyo inasemekana vilikua na sumu.
Mama yake mzazi ameongea na kusema
Madaktari wasingeweza kuokoa maisha yake, kunywa hizo dawa ni sawa na
kujisogeza karibu na kifo, zinasababisha pia mwili upate joto kupitiliza
na kusababisha pia ini kushindwa kufanya kazi.
Eloise
alipoanza kuona hali iko tofauti baada ya kunywa dawa alikwenda
hospitali mwenyewe lakini ikawa imeshaharibu tayari, alichelewa kwenda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni