Obert funga.
Kahama.
27/04/2015.. Jeshi la polisi.
Jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia katika halmashauri ya mji wa kahama mkoani hapa, kimemkamata aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji cha Busulwangili kata Bugarama Katika halmashauri ya msalala Bw,kinasa Jumanne [CCM] ambaye alifunguliwa kesi na mke wake KAH/RB/5093/2014.
Mwenyekiti huyo aliyekuwa anadaiwa kumpiga mke wake mara kwa mara na kusambaratisha familia nyenye watoto 7 huku akimpiga mke wake na kufukuza nyumbani kwa lengo la kuoa mke mwingine ambaye alishamchumbia toka 13/4/2014.
Akizungumza katika ofisi za shirika la haki za binadamu[SHIHABI]lililopo wilayani hapa Bi,Mary Said ambaye alikuwa mke wa mwenyekiti huyo alisema alikuwa na tabia ya kunipiga kuninyang’ang’anya mazao,mifugo na kuchoma moto nguo zangu mpaka nikaamua kuondoka na watoto 4.
Bi,Mary aliendelea kueleza mashitaka ya mwenyekiti ya kuwa hadi sasa mtoto wao Helena Kinasa[13]aliyekimbia nyumbani kwa ugomvi wa kunyang’anywa kila kitu ajaonekana hadi sasa licha ya kutoa taarifa sehemu mbalimbali.
‘’wakati ni mume wangu kabla ya kujulikana ya kuwa ana mke alikuwa ni mtulivu lakini alipoamua kuoa mwanamke huyo ndipo visa vilipoanza kwa kuuza ngo’mbe,mbuzi na mashamba na watoto wakifukuzwa shule kwa ajiri ya michango alikuwa hatoi na kunisukumia mimi’’alisema Mary.
Mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za binadamu[SHIHABI] Bw,Solomon Kitigwa alisema tunashukuru kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na Mwanasheria wetu Bw,Juma Mpondi kwa kumtendea haki Mary Said toka 23/9/2014 alikuwa amechanganyikiwa kwa mambo mengi ikiwa na kupoteza watoto wake 2.
‘’tunataka tufanye mrejesho wa yale yaliotokea kijijini busulwangili kwa uonezi aliofanya na sheria ya udhalishaji,kupiga,mirathi pamoja na makosa yote yanayomkabili kwa aliyekuwa mke wake 2014 na kufikia hatua kumfukuza na yeye kuchukua mali zote walizochuma na kutokomea kusikojulikana mpaka amekamatwa’’alisema.
Hata hivyo shirika la kutetea haki za binadamu SHIHABI ikishirikiana na jeshi la polisi limesema lina makesi zaidi ya 345 ya ambayo litayashughulikia kwa kutenda haki kwa kila upande kuwe sawa baadhi ya kesi ambazo zinafanyiwa mnyambulisho kwa kuwapeleka mahakamani ni udhalilishaji,mirathi,kutelekeza watoto,ugomvi,unyang’anyi,kutowasomesha watoto na fumanizi.
MWISHO
| BARABARA YA BULIGE kuelekea kijijini kwao MARY DAID |
![]() |
| WALIOTELEKEZWA |
![]() |
| MIFUGO ILIOUZWA |
![]() |
| MKE MPYA |



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni