Obert funga.
Kahama.
24/04/2015. Sawamu-kata
Shirika la Shdepha+ Tawi la kahama mkoani hapa lenye juhudi ya kupinga mauaji ya vikongwe,maarbino na watoto waishio katika mazingira magumu limewaunga mkono wazee wa kata ya mungula kwa ufunguzi wa tawi la sauti ya wazee mungula ‘’sawamu’’yenye kauli mbiu ya wazee ni hazina ya busara.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa [sawamu]mwenyekiti wa Shdepha+ wilaya ya kahama Bi,Ferister James alisema kumekuwepo na mtazamo hasi kwa haki za wazee kuonewa,kunyimwa matunzo,kunyan’ganywa ardhi,kunyanyaswa kwenye mirathi na kuporwa mashamba bila kufuata sheria inasema jambo gani.
‘’ifikie wazee hasa wanawake wenzangu ninyi ndiyo munaonewa zaidi kwa kunyimwa matibabu,mauaji ya macho mekundu,athari za mirathi, matunzo ya uzee na umuhimu wa uwepo wenu wazee kama hamkuwa vijana wa enzi zile pia heshima na busara hampati kwa nyakati sahihi’’alisema Ferister
Awali mwenyekiti wa [sawamu]kata ya m ungula Bw,joseph mwikoko alisema kuanzishwa kwa kikundi hicho ni mara baada ya kuona matendo na nyendo za udharirishaji kwa wazee mbalimbali wakifanyishwa kwa mlengo wa kutouona umuhimu wa haki za wazee ukifanyiwa ipasavyo.
Bw,mwikoko alisisitiza ya kuwa wilaya ya kahama ndiyo yenye mtindo wa kiuonevu kwa wazee hususani mauaji ya vikongwe,arbino,rushwa ya ardhi na haki stahiki ya matibabu licha ya kuwa na wazee wa aina 2 ya wazee wakulima na wazee wafanyakazi pia nawaliostaafu.
‘’tumekuwa na ubabaishaji wa matibabu katika hospitali ya halmashauri ya mji wa kahama, kila mara tunaambiwa dawa hakuna idara ya afya na uongozi wa halmashauri haitutendei haki kwa mujibu wa haki na sheria iliopo katika katiba ya 1977 na katiba pendekezwa ya 2015’’ Alisema mwikoko.
Naye mgeni rasmi wa ufunguzi huo Bw,Paul Ntelya ambaye pia ni katibu wa umoja wa wazee wilayani kahama[uwaka]aliwasihi wazee hao kuwa na umoja wenye mitadhamo ya chanya na hasi pasipo kuulinda uzee ambao ni wosia wa vizazi vijavyo kama kauli mbiu ya [uwaka] uzee ni hekima,uzee ni busara na uzee ni dawa.
‘’’Napenda niwajulishe vyema umoja wa wazee wilaya ya kahama ulianzishwa miaka 4 iliopita lakini umesajiliwa kihalali kwa usajili wa namba S.A.18560-2013/14 kwa kuheshimu uzawa wa kahama katika ukanda wa ziwa kutokana na uonevu,rushwa na mauaji mbalimbali yanayofanyika mkoani shinyanga na mikoa mingineyo’’’alisema Ntelya.
Bw,Ntelya aliongeza ya kuwa nawashukuru kwa kufikiria maendeleo ya kata ya m ungula hususani wilaya hii kwa kuunda kikundi hiki pia kutetea na kuulinda uzee ambao ni hazina na busara nchini kote licha ya idara ya afya ya kahama kutofanya uhalali wa mzee apate matibabu nyakati za magonjwa nyemelezi lakini ofisini kumekithiri rushwa na neno dawa hakuna.
Uwaka katika vikao mbalimbali imeweka mikakati ya kuwakutanisha viongozi wa ngazi zote kwa kukosoa utendaji usio mwema pia kuulinda maadili ya asili ya utamaduni wa sisi wazawa na wageni iliwapate utofauti wa maendeleo ya mkoani hapa bila kuweka ukanda huu kuwa ni shamba la bibi.
Aidha afisa mtendaji wa kata ya mungula Bw,Waitara Kishamori aliupongeza uongozi wa ‘’SAWAMU’’ulioteuliwa kwa utendaji wa kuchuja mabaya na mazuri ya uzee unaotendewa na wadau,mashirika,serikali na wahisani wanaopigania haki za wazee zilizoainishwa kihalali katika katiba ya 1977 kwa kupinga mauaji,ukandamizaji,mirathi na matibabu yasio na tija kwa wazee.
Viongozi walioteuriwa katika mchakato wa wajumbe wa kamati kuu tendaji ya [sawamu] mwenyekiti kata ni Joseph Mwikoko--Mwenyekiti msaidizi ni Modester Maziku--katibu mkuu Nestory Kija Ntugwa---Katibu msaidizi ni Magdalena Lyadadi,,ikiwa na wajumbe zaidi ya 42 waliopo katika kata ya mungula na mitaa ya Bukondamoyo,Inyonga,Inungu.
…………………..MWISHO…………………..
| MZEE munde akipinga UONGOZI ULIOPENDEKEZWA WA sawamu |
| |
| Gigwa ntobu akiunga mkono UONGOZI uliopendekezwa |
| Mwenyekiti wa Shirika la SHDEPHA+ Tawi la kahama Bi,Ferister James Akiongea na wazee hao |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni