Obert funga.
Kahama.
27/04/2015. TANROADS
Uongozi wa kituo cha radio cha kahama fm kilichopo wilayani hapa mkoa shinyanga kilichotangaza 27/4/2015 saa 21:00 usiku ya kuwa wanasisa wanakichafua kituo hicho kwa maneno ya uongo katika taarifa zake za habari kuwa si za kweli kama zilivyosomwa siku hiyo kwa tamko la meneja mkuu wa kituo hicho Bw, Marko Mipawa.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Madata Mgeja amepinga vikali Taarifa ya habari iliotangazwa na kituo hicho kilichotangazwa 6/4/2015 ya kuwa ‘’mgeja ampongeza wakala wa barabara ya tanroads kwa kulekebisha barabara za kuridhisha’’.pia ‘’habari ya wachimbaji wadogo waanza kuondoka mwabomba’’na habari nyinginezo.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taarifa hiyo alisema ukweli nilikwenda vijiji vya kata ya ulowa na ulewe jambo niliolizungumza tofauti na ambalo nambiwa limetangazwa katika kituo cha radio naomba nieleweke vyema au soma gazeti la jambo la 5/4/2015 utagundua linichomanisha katika harakati zangu za kufanya ziara za halmashauri ya ushetu.
Mgeja imezitaka radio za jamii zifuate utaratibu wa taaluma halisia bila kufanya kazi kwa kufuata siasa za maji taka ambazo hazina msingi katika jamii ya watanzania tunaejivunia amani na utulivu wa taifa lenye mlengo wa kuwa huru kwa namna yeyote kwa kufuata ibara ya katiba 17-19 ya jamhuri ya muungano Tanzania ya 1977.
Awali kulikuwa na ratiba ya mwenyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga kufanya mikutano ya chama katika kata za halmashauri ya ushetu wilayani kahama 27-28/3/2-15 ambapo alizungumzia madaraja zaidi kutofanyiwa ukarabati maalumu wa barabara za tanroads na barabara zinazokarabatiwa na halmashauri ya ushetu.
Hata hivyo mwenyekiti huyo alizitaka halmashauri zote 3 za wilaya ya kahama mkoani humo kushirikiana na wakala wa barabara Tanzania[tanroads] kutatua matatizo yanayoikabili miundombinu wilaya hii kunatokana na usimamizi dhaifu wa kitengo cha tanroads ikiwa na halmashauri zote 3 kuyaacha magari ya mizigo,mifugo isiwe inafuata masharti na vigezo vya barabara za halmashauri.
Mgeja alisisitiza ya kuwa ushirikiano wa halmashauri ya mji wa kahama uliofanya na kampuni ya buzwagi gold mine [ACACIA] ndiyo ufanyike na halmashauri za msalala na ushetu pamoja na tanroads kwa barabara zilizo na usumbufu na uhalibifu ikiwa na mitalo,uchafu,madaraja sumbufu na michanga inayojaa barabarani.
Kukabiliana na barabara za Tanroads zenye uharibifu mkubwa ambazo zinatakiwa zifanyiwe ukarabati wa kiwango kikubwa ni barabara ya kahama-bulige,kahama-busoka,kahama-chambo,busangi-segese,kahama-ulowa na barabara nyinginezo ambazo zitaiweka kahama katika hadhi yenye mapato makubwa katika mkoa wa shinyanga.
Alipoulizwa wakala mkuu wa TANROADS mkoa wa shinyanga Bw,Sebastian kifafa alisema wewe ndiyo unanieleza hayo ya kahama mimi sina taarifa ya mgeja kusifia barabara za tanroads ambazo azijafanyiwa matengenezo zaidi ya miaka 4,kama mimi sina hata mawasiliano naye pia anastahili pongezi mkurugenzi wa halmashauri ya ushetu.
Aidha Bw,Kifafa alisema tuna subiri serikali kuu kufanya tathimini ya ya bajeti ikiwa na mgawo wa hazina ili tupate uwelekeo wa taratibu za matengenezo,malekebisho ya barabara zetu kwa kiwango kinachotakiwa katika nchi hii ni utawala na utaratibu halisia.
…………………..MWISHO………………
| BARABARA ZA TANROADS KAHAMA---BULIGE |
| BARABARA ZA TANROADS .....KAHAMA---CHAMBO |
| BARABARA ZA TANROADS AMBAZO ZINASIFIWA KUWA ZINARIDHISHA |
| BARABARA ZA HALMASHAURI YA MJI WA NKAHAMA |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni