ANASWA AKIIBA MAHINDI.......NASEMA KULA YOTE ULIYOJAZA KWENYE GUNIA
Akilazimishwa kula mahindi hayo.
Jamaa ambaye jina
halikuweza kupatikana mara moja, amejikuta akionja joto ya jiwe baada ya
kudaiwa kukutwa akiiba kwenye shamba la mahindi hivyo kulazimishwa kula
mahindi mabichi.Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni kwenye
Kata ya Miembeni, Bukoba mkoani Kagera na kuibua gumzo kubwa.
Kwa mujibu wa shuhuda
wetu, baada ya kumnasa kijana huyo akiiba mahindi aliyoyajaza kwenye
gunia, wamiliki wa shamba hilo walimuamuru kukaa chini na kuyala yakiwa
mabichi hadi yaishe, kitendo ambacho jamaa huyo alikubaliana nacho.
Akila maindi hayo ili kuepuka kichapo.
Ilielezwa kwamba, katika
hali ya kushangaza, kijana huyo hakukataa wala kuonesha kutetereka
kwani alianza kuyala hadi alipoamriwa kuacha na kuambiwa aondoke.Katika
habari hiyo iliyoripotiwa na Mtandao wa Harakati, kijana huyo alionekana
kuwa na matatizo ya kutosikia vizuri wala kuongea kwa maana ya kuwa ni
‘bubu’.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni