Mmoja wa vijana walionaswa kwa ujambazi jana akiwa na msichana anayedaiwa kumvisha pete hivi karibuni.
Vijana hao wakiwa chini ya ulinzi baada ya kutiwa nguvuni.
*************
Mmoja
wa vijana wanne walionaswa jana katika tukio la ujambazi eneo la Mataa
ya Red Cross katikati ya Jiji la Dar es Salaam, hivi karibuni anadaiwa
kumvisha pete msichana mmoja ambaye ni mchumba wake.
Vijana
hao walitiwa nguvuni na Jeshi la Polisi jana baada ya kuvamia na
kumpora fedha raia mmoja wa kigeni eneo la Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Baada
ya kufanya tukio hilo, vijana hao walifanikiwa kukimbia na gari
walilokuwa nalo ila kulikuwa na msamaria mwema mmoja aliyeona tukio hilo
ambaye aliweza kufukuzana nao akiwa na gari yake na kufanikiwa kuwapita
mbele na kuwazuia na hivyo kushindwa kupita na gari walilokuwa nalo
ndipo askari kufika na kuwaweka chini ya ulinzi.
Vijana hao wanne ambao ni watanashati na ni vigumu kudhani kuwa wanaweza kujihusisha na vitendo vya ujambazi, baada ya kukamatwa na polisi walikutwa na bunduki mbili

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni